Billboard ni moja kati ya partners wakubwa sana kwenye muziki duniani, pia wanahusika na upangaji wa chart kubwa zaidi duniani za muziki kupitia mtandao wao, leo ninayo hii kutoka kwao ambapo wameitoa list ya wasanii 10 wanaoanza kufanya vizuri kwenye muziki, jina la star muimbaji Tekno limewekwa kwenye list hiyo.
Wasanii hao ni kutoka sehemu zote duniani na kupitia list hiyo, Tekno ndiye msanii pekee kutoka Afrika aliyetajwa kuwemo kati ya wasanii 10 wa kuwaangalia zaidi mwaka 2017 na wote wanafanya muziki wa Hip-Hop na R&B.
jarida la Billboard pia limethibitisha deal iliyosainiwa kati ya Tekno na kampuni kubwa ya kusambaza muziki duniani “Sony Music” ambapo yeye atakuwa chini studio za Columbia Records.
Billboard wameandika:
“Tekno tayari ana hits kali nchini kwake Nigeria, na Columbia Records wanafahamu hilo, huyu ni msanii mzuri, na ana sauti yenye kuvutia kila mara. Mfano wimbo wake bora zaidi “Pana,” ambao umeshatazama zaidi ya mara milioni 13 kupitia YouTube na wasanii wengine wakaifanyia remix mara nyingi.”
Sio rahisi kumzuia muimbaji huyu kuingia kwenye mainstream kwa jinsi wimbo wake unavyovuta hisia: jaribu kufumba tu macho halafu msimamizi wa vipindi vya radio ambaye yuko smart aukate wimbo wa Drake “Too Good” halafu aipige Pana.” – Billboard
- Kehlani
2. Aminé
3. YFN Lucci
4. Leela James
5. Kodie Shane
6. Princess Nokia
7. Guordan Banks
8. Tekno
9. Khalid
10. H.E.R.
ANGALIA SHOW YA MR BLUE AKIWA MBEYA HAUTAKIWI KUKOSA HIIII
Comments
Post a Comment