Likija swala la kuripoti ishu za usajili BBC wamejipatia standard ya juu kwasababu mara nyingi huwa hawakosei juu ya ishu za usajili. Sasa hivi wameripoti kwamba Mourinho amebadirisha mawazo yake juu ya kumsajili mchezaji Victor Lindelof kutoka Benfica.
Imeripotiwa sana kuhusu mchezaji huyu kuelekea kujiunga na club ya Manchester united ambapo ali saini hadi jezi ya Manchester ambayo alikuwa nayo shabiki mmoja.
BBC wameandika kwamba Jose ameshawishiwa kwa uzuri wa Rojo na Jones kwenye ulinzi sehemu ya kati kati kiasi cha kubadirisha maamuzi ya kutaka kumnunua mchezaji huyo. Jose pia ana imani kubwa na Eric Bailly, Chris Smalling na Daley Blind.
Lindelof ilitoka taarifa kwamba zingetuma Euro millioni 45 ili awezeze kuhamia Manchester United kutoka Benfica, Kiasi hiki kingekua kikubwa zaidi kwa Benfica tangu waanze kuuza wachezaji.
Comments
Post a Comment