Simu za Smartphones zimekuwa ni kati ya vitu vinakimbizana na teknolijia kila kukicha, na ni moja kati ya vifaa ambavyo vimekuwa seheme ya maisha ya karibu asilimia 70 ya watu duniani lote, kuna wakati simu tunazomiliki zimekuwa zinatoa majibu ya wewe ni mtu wa aina gani.
Simu zimekuwa zikitengenezwa kuleta ushindani wa teknolojia lakini kupima uwezo wa kifedha wa watumiaji na mapenzi.
Kwa mujibu wa The Merkle wamezitaja aina 5 za simu ambazo mpaka kufikia mwezi December 2016 zimekuwa ni simu zilizovunja rekodi ya kuuzwa kwa bei ya juu kuliko simu nyingine zozote duniani. Japokuwa hizi simu ni za kawaida ila tu zimekuwa zikiongezewa urembo wa madini ya thamani kubwa ili kuzipa muonekano wa kipekee .
5.- GOLDVISH LE MILLION ($1.3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 2.8)
Sifa ya hii simu ukiishika kama sio mmliki wake inapiga kelele zenye sauti ya kuonesha imeibiwa. Cover la nje lote limeunda kwa Almasi ya Karat 120, na cover la ndani limeundwa kwa dhahabu ya kutosha.
4.- DIAMOND CRYPTO SMARTPHONE ($1.3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 2.8)
Simu hii imeundwa na mtaalmu wa madini aitwaye Peter Aloisson na ilitoka kwa mara ya kwanza mwaka 2006, Simu hii ya Diamond Crypto Smartphone iliundwa kwasababu maalumu za kutunza siri, kwa mujibu wa watengenezaji wake. Simu hii hutumia OS ya Windows CE kama mfumo mkuu wa uendeshaji wake. Simu hii imeundwa kwa madini ya Almasi ambapo kuna vipande 50 pia vya Almasi ya blue.
3.- AMOSU CALL OF DIAMOND IPHONE 6 ($3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 6.5)
Alexander Amosu ndiye mtengenezaji wa simu hii ambaye mwanzo alikuwa akifanya biashara ya kuuza ringtone za simu. Kwasasa anaziongezea urembo simu na kuziuza kwa mastaa wa muziki, wacheza filamu, wanamichezo pamoja na watu maarufu wenye uwezo mkubwa kifedha.
The Call of Diamond ni simu aina ya iPhone 6 ambayo imenakshiwa kwa Gold ya Karat 18 kwenye cover lake la ndani wakati kwa nje imewekewa vipande vya Almasi vinavyofikia 6,127 na inamaliziwa na logo ya Cupertino moja ya makampuni makubwa duniani.
2.- BLACK DIAMOND IPHONE 5 ($15 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 32.6)
Kama ulidhani dola milioni 3 ni nyingi kununua simu sasa kutana na hii, inaitwa Black Diamond iPhone 5. Simu hii imeundwa kwa Gold inayifikia Karat 26, Almasi iliyotiwa rangi nyeusi pia imeongeza urembo kwenye simu hii. Black Diamond inatengenezwa na kampuni ya mfanyabiashara kutoka China anaitwa Stuart Hughes.
1.- FALCON SUPERNOVA IPHONE 6 ($100 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 217.8)
Bila shaka umeona gap lililopo kutoka simu iliyoshika nafasi ya pili! Hii ni iPhone 6s ambayo kila kitu kilichopo kwenye simu hii ni madini ya Almasi, Gold pamoja na Ruby. Mzigo unaitwa The SuperNova pamoja na bei hiyo bado unaambiwa hii sio simu ya gharama kati ya zilizowahi kuundwa.
Comments
Post a Comment