Kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV sasa kutaitwa SHILAWADU. Mabadiliko ya kipindi hicho cha burudani yataenda sambamba na ujio wa Shilawadu Ubuyu Tour ambapo watangaji wa kipichi hicho, mastaa pamoja mashabiki watapata fursa ya kupanda basi hilo la tour na kukutana na mastaa wao huku kipindi kikirekodiwa.
Qwhisar Thomson mmoja kati ya watangazaji wa kipindi hicho
Qwhisar Thomson mmoja kati ya watangazaji wa kipindi hicho
Akizungumza na waandishi wiki hii mmoja kati ya watangazaji wa kipindi hicho, Qwhisar Thomson alisema kipindi hicho kimeenda mtaani ili kutoa shukrani kwa mashabiki pamoja na kuwapa fursa ya kukutana na mastaa ambao wamekuwa wakihojiwa kila siku.
“Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu, mastaa pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa pamoja na sisi kuanzia mwanzo mpaka sasa hivi,” alisema Qwhisar “Lakini katika namna ya kuwashukuru zaidi tunaenda mtaani na tour basi yetu kuwapa fursa mashabiki ya kukutana na mastaa wao pamoja na kuwauliza yale ambayo wamekuwa wakiyauliza kupitia mitandao ya kijamii.,”
Qwhisar alisema tuor ya Shilawadu Ubuyu Tour itaanza Desemba 24 kwa wakazi wa wilaya ya Temeke, baada ya hapo itaingia Kinondoni pamoja na Ilala.
Pia kipindi hicho kimetambulisha bidhaa yake mpya ya ubuyu wenye jina la kipindi chao ‘SHILAWADU’.
Comments
Post a Comment