Msanii wa muziki kutoka Aljazzirah Entertainment, Killy ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo Rudi, Jumamosi hii amevunja ukimya kwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Nikwambie’. Video imeongozwa na director mkongwe nchini Adam Juma.
Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.
Comments
Post a Comment