Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea tena leo December 24 kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja tofauti Tanzania, Simba walikuwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wao wa marudiano wa mzunguuko wa pili.
Simba ambao mwishoni mwa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu soka Tanzania bara walianza kukumbana na wakati mgumu, leo December 24 wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 49.
Kwa dakika zote 90 Simba walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 52 wakati wapinzani wao JKT Ruvu waliutawala mchezo kwa asilimia 48 tofauti ambayo inaonesha kuwa mchezo haukuwa rahisi kwa Simba licha ya kupata ushindi, ushindi huo umeifanya Simba kuwazidi wapinzani wake Yanga kwa tofauti ya point 4 wakiwa leo wamefikisha point 41.
Comments
Post a Comment