Skip to main content

Posts

Showing posts from 2017

MASWAIBU YA MKE WA MTUU SEHEMU YA KWANZA

STORY BY ABDALLAH JONGO STORY INAHUSU MASWAIBU YA MKE WA MTU SEHEMU YA KWANZA Whatsapp...0757357341            Ilikua muda ya saa kumi na moja alfajiri katika kijiji cha Koromije kwenye nyumba ya amina kulitokea na zogo kubwa ambalo lilileta sintofahamu kwa bwana Athumani na binti Amina kwani siku hiyo bwana Athumani alikua amesikia maneno kutoka kwa jirani zao kua mke wake Amina hua anaaga nana kwenda kuswali alfajir kumbe anaenda kwa bwana john kitendo cha mmewe kumkataza kuto kwenda kuswali aliona kama anaonewa hii au atendewi haki....................................           Ilichukua takiribani saa nzima la zogo mpaka watu walio kua wana pita kusikia mizozo ilio kua ina endelea kwa bwana Athuman na watu wakalazimika kuonga hodi kujua tofauti zao lakini hilo swala likazungumzwa na wapita njia mpaka wakafikia mua faka ilipita takribani wiki moja wakiishi kwa kutokua na mazungumuzo madhuri katiyao mwanamke aliomba ruhusa ...

KWENYE ENEWZ 10 MAY, 2017 Snura Shilole ananibania

Msanii wa kizazi kipya snura mushii amesema kama mashabiki zake wanavyopenda kuona korabo yake na shilole naye hivyo hivyo jana jionii kwenye Enewz ya EATV alifunguka kua Shilole anamkwepa sana hata zikitokea show anakwepa ila yeye snura amesema yupo tayari kabisa hatakusimama steg moja naye TAZAMA HAPA

ENEWZ MAY 08, 2017 Dogo Janja amwagia sifa Harmorapa

Msanii wa kizazi kimpya alimaarufu kama dogo janja amemwagia sifa kede kede msanii harmorapa kua harmorapa yeye hatafuti kiki ila kiki zina mfuata yeye ukiangalia kwenye tukio la kutolewa bastora kwa aliekua waziri wa habari nape yeye alikimbia watu wakaweka kama kiki alifanya harmo rapa wakati sio kweli.nakuzihilisha kua anamkubali mpaka kwenye cm yake ananyimbo ya harmorapa kiboko ya mabishoo.dogo janja anayefahamika kwa kibao chake kipya alicho toa jana jumaa tano cha kinacho itwa ukivaanguo gani unapeneza.

HATIMA YA WATUMISHI HEWA LEO RAIS MAGUFURI APOKEA RIPORT LEO DODOMA KWENYE UKUMBI WA CHIMWAGA MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Soma Taarifa kamili:

BURUDANIPicha: Tazama makazi mapya ya Jay Z na Beyonce

Jay Z na Beyonce ni moja ya couple katika Ulimwengu wa burudani, yenye uwezo wa kupata chochote wanachokihitaji katika kufurahia maisha yao. Wawili hao wamedaiwa kununua jumba la kifahari mjini Los Angeles. Kwa mujibu wa Page Six, maamuzi ya wawili hao kununua jumba hilo la kifahari, limetokana na kubadilisha mazingira kutoka New York ambapo wanaishi sasa, kwa ajili ya kuwakaribisha watoto wao mapacha ambao wanatarajiwa kuzaliwa Juni mwaka huu. Jumba hilo linadaiwa kuwagharimu kiasi cha dola milioni 135 likiwa lina vyumba nane vya kulala, mabafu 11, madirisha yasiyopitisha risasi, chumba cha habari, sehemu ya studio, gereji yenye uwezo wa kuchukua magari 15 kwa wakati mmoja na mengine. Kama ni kweli Jay na Queen Bey watahamia kwenye jumba hilo watakuwa ni majirani wa mastaa wengine kama muigizaji, Salma Hayek, muimbaji Tom Jones na bosi wazamani wa Disney, Michael Eisner.

Wizara ya afya yaongeza muda wa kubadilisha cheti cha chanjo ya homa ya manjano

Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya. Wizara inapenda kutoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kama ifuatavyo. Kabla ya kuanza matumizi ya vyeti vipya, wastani wa wasafiri 800 walikuwa wanapatiwa chanjo kwa mwezi kupitia vituo vilivyoruhusiwa na Wizara. Baada ya kuzindua vyeti vipya na kuongeza udhibiti wa vyeti feki idadi ya wanaopata chanjo imeongeza kutoka 800 hadi 2,445 kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la mara 3 ya waliokuwa wanachanja hapo ...

Mwanamke mwenye uzito mkubwa alivyopungua India

Bi Abd El Aty kutokea Misri alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Saifee miezi miwili iliyopita, ili kupungua kutoka uzito wa kilo 500 hadi 250 kwa sasa. Hospitali hiyo imesema mama huyo, sasa anaweza kuketi kwenye kiti cha magurudumu na kukaa chini kwa muda kinyume na hali ya awali. Abd El Aty alifanyiwa upasuaji unaojulikana kama ‘bariatric’ na kundi la madaktari wa India wakiongozwa na Daktari Muffazal Lakdawala. Upasuaji wa ‘Bariatric’, hufanyika wakati mtu anapokua na unene kupita kiasi na ikiwa hali hiyo inatishia maisha yake. Hospitali hiyo inasubiri mwanamke huyo kupunguza uzani zaidi ili kuchunguzwa zaidi kuhusu hali ya kiharusi chake alichokipata tangia mdogo. ANGALIA HISTORIA YA LUCKY DUBE HAPA

Rais Magufuli amempigia simu Mwana FA

Jioni ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo   Hamisi Mwinjuma   ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la   Mwana FA , alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   John Pombe Magufuli   kumpigia simu. Mwana FA   ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya   Dume Suruali   amethibitisha kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake. Kupitia ukurasa rasmi wa   twitter   wa staa huyo uliyokuwa verified aliandika   “nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais   @MagufuliJP   kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa   #DumeSuruali ..”

LORD EYEZ AIKANA LEBO YA BANA YA BARAKAH THE PRINCE

Lord Eyez ameonekana kukataa kiaina kusainiwa na lebo ya BANA ambayo inamilikiwa na Barakah The Prince. Rapper huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’ aliomshirikisha Jux, amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumsaini yeye kwakuwa ni mkubwa zaidi. “Kuna makubaliano yangu na Barakah chini ya BANA huo wino ni mimi na yeye, huo wino hamhusu mtu mwingine yeyote. Nafikiri kwa sababu hakuna mtu yeyote anaweza kuniown Lord Eyez. Hakuna mtu anaweza kumsaini Lord Eyez coz am too bigger for that,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. “Nafikiri maswali yanakuwa mengi kwasababu labda watu hawakuniona Lord Eyez, hawakunipata nikizungumza. Unajua mimi sio mtu wa pele pele, mimi sio mtu wa kiki, mimi sio mtu wa media, mimi napenda muziki wangu uwe mkubwa kuliko mimi,” ameongeza.

Tunda aeleza jinsi sakata la dawa za kulevya lilivyobadili maisha yake

Video queen Tunda amedai kutajwa kwake kwenye orodha ya wanaohusika na dawa za kulevya kumempa changamoto ya kuaminika nyumbani kwa wazazi wake. Mrembo huyo amekiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa tangu kutajwe kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu kumuelewa. “Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. Maisha ya mitandaoni nimeacha. Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi kueleweka na wazazi,” alisema Tunda. Aliongeza, “Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii madawa ya kulevya.” Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Manara awajibu Yanga baada ya kupinga malalamiko ya Simba kwa mchezaji wa Kagera Sugar

Baada ya kamati tendaji ya Yanga kupitia kwa mjumbe wake Salum Mkemi kutanganza kupinga malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji wao Mohamed Fakih kwenye mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba, afisa habari wa Simba Haji Manara ametoa taarifa rasmi akiwataka Yanga kutulia. Kuna taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria. Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano. Klabu ya Simba inawaa...

Bashe awasha moto bungeni sakata la utekwaji watu

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema hawezi kulifumbia mambo jambo la watu kutekwa na watu wasiojulikana. Bashe ameyaanisha hayo Jumatatu hii na kusema kuwa na yeye ni mmoja wa watu wa waliotumiwa ujumbe wa vitisho ambao ulisema atafanyiwa vitendo vibaya popote alipo. Aidha Mhe Bashe ameeleza kuwa kuna kikundi kilicho chini ya idara ya usalama wa taifa kinachoendesha matukio hayo na kinaharibu heshima ya serikali na chama na ameomba ikiwezekana Bunge liunde ‘Committee’ ya kuchunguza jambo hilo. Sambamba na kuzungumza bungeni hakuishia hapo katika mtandao wa tweeter ameandika: “Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.”

Mimi Mars adai Lulu na Wema waliwahi kukataa kumpa shavu kwenye movie

Marianne Mdee aka Mimi Mars amepitia vikwazo vingi katika kutafuta tobo kama ambavyo wasanii wengine wamepitia licha ya yeye kuwa mdogo wake na Vanessa Mdee. Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Mimi alisema Lulu na Wema Sepetu waliwahi kumtosa kumpa shavu kwenye movie. “Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini, Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga chini fulani hivi but it’s okay,” alisema. Hata hivyo Mimi hana kinyongo nao kwakuwa kipindi hicho alikuwa hajulikani na anaona ni kitu cha kawaida. Anasema wawili hao kwa sasa ni marafiki zake.

Tumeshtushwa na tukio la Roma, lazima tujue kiini chake – Dkt Mwakyembe

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amesema tukio la kutekwa kwa Roma na wenzake watatu limewashtua. Ameda kuwa hilo si jambo lililozoeleka Tanzania na kwamba ni lazima wafuatilie kujua kiini chake. Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Dkt Mwakyembe amesema tukio hilo linaweza kuwa limefanywa na watu wachache kwaajili ya kuvuruga mambo. “Mimi nawathamini sana vijana wangu hawa,” amesema Dkt Mwakyembe. “Hawa ni stars, hawa ndio wanainbrand Tanzania. Huyu ni bendera ya Tanzania, siwezi kukubali tukachezeachezea watu hawa kwasababu zozote zile, ndio maana nasema tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunaviruhusu vyombo vya upepelezi ambavyo vitafuatilia kwa ukaribu sana tupate majibu ya kile kilichotokea,” ameongeza. Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa wizara yake ipo kwaajili ya wasanii na itawalinda kwa namna yoyote na kwamba pale watakapoona hatari yoyote wasisite kumjulisha. Amesema anachosubiri ni majibu ya upepelezi ulioanza ...

‘Acha Nikae Kimya’ yamponza Diamond kwa Gwajima ‘Yala! yala! mwenzenu nimeyatimba’

Diamond ameingia choo cha kike kwa askofu Joseph Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You’ amejikuta matatani baada ya kuachia wimbo mpya ‘Acha Nikae Kimya’ ambao umepokelewa vibaya na mashabiki wengi wa muziki. Katika wimbo huyo ametajwa askofu Gwajima kitu ambacho kimemchukiza mchungaji huyo maarufu katika mitandao ya kijamii. “Kesho Ibada itakuwa LIVE on YOUTUBE kuanzia saa nne na nusu, kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Kibo Dar es Salaam. Link itakuwepo kwenye Bio yangu. Usikose.,” aliandika Gwajima Instagram akiambatanisha na picha (hapo juu Baada ya ujumbe huo wa Gwajima, Diamond amerudi upya kuomba radhi kuhusu kumhusisha mchungaji huyo kwenye wimbo wake. “Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba ….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasi...

Young Killer aeleza alivyojisikia baada ya Diamond kunukuu mistari minne kwenye nyimbo zake 3 tofauti

Diamond Platnumz ni shabiki mkubwa wa Young Killer. Na hitmaker huyo wa ‘Marry You’ si mtu anayesikiliza nyimbo za Msodoki juu juu tu, bali kwa undani kiasi cha kushika mistari kadhaa. Mwishoni mwa wiki, Diamond alionesha wazi kuzimia mistari konde ya rapper huyo wa Mwanza kwa kuandika minne kwenye post zake nne tofauti za Instagram na Twitter. Mistari ya Young Killer ambayo Diamond ameiandika kwenye post zake za Instagram ni pamoja na: 1. Asa Unataka kuwa mimi na mimi ntakuwa nani….?   (Sinaga Swagga (Part1) 2. Naskia Usingizi ni Mbolea ndiomaana tukilala tunaota…?   (Sinaga Swaga Remix) 3. Ukiona Nina changamoto changa Unga tusonge Ugali… Mwisho wa siku wote tunashiba, na Mambo yanakuwa shwari (Sinaga Swagga 1) 4. Shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengine (Kumekucha f/ Mr Blue) “Binafsi nafarijika sababu ni [Diamond] mtu ambaye ana fan base kubwa kwahiyo anapokuwa ameshow love kwa kitu kama hicho kupost mistari yangu hata mashabiki wake pia wanakuwa wanan...

Joh Makini na Davido washoot video ya collabo yao

Hatimaye Joh Makini na Davido wamefanikiwa kushoot video ya collabo yao. Video hiyo imefanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Kupitia Instagram ni Davido ndiye aliyetoa habari hizo njema kwa kuweka picha akiwa na Joh pamoja na warembo sita. “Back to work !! On set     shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ     x NAIJA   ,” ameandika. Wimbo huo una takriban mwaka na nusu tangu urekodiwe na ni video pekee iliyokuwa inasubiriwa ili uachiwe rasmi.

Mkwe wa Trump ambaye ni mshauri wa rais aanza ziara nchini Iraq

Mshauri mkuu wa rais Donald Trump ambaye pia ni mkwe wake Jared Kushner amefanya ziara nchini Iraq kwa mara ya kwanza wikiendi hii. Afisa mmoja kutoka Ikulu ya Marekani ameiambia CNN kuwa Jared amesafiri na Jenerali Joseph Dunford katika ziara hiyo ambapo wanatarajiwa kurudi mapema wiki hii. Siku chache zilizopita mshauri huyo na mkewe Ivanka Trump ambaye ameteuliwa kukalia kiti cha msaidizi wa rais asiyelipwa walitajwa kuwa na utajiri wa takribani dola milioni 740.

UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema

Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono wanabalehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo. Professor  Jennie Noll   aliliambia Jarida la   Adolescent Health:  >>>   “ Watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa au kubakwa hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida. “ Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe. Wanasaikolojia hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovari na matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazing...

Tizama macth live kati ya liverpool na everton

Moja kati ya majiji yenye historia ya mchezo wa soka nchini England ni pamoja na Merseyside, jiji ambalo linatoa team kama Liverpool   na hata  Everton . Huwa kinanuka mbaya  timu hizo zinapokutana kutokana na upinzani uliopo baina yao na mambo mengine kibao. Leo April 1  Everton   ni mgeni wa  Liverpool .  inakupa nafasi ya kuitazama LIVE game hiyo kwa kubonyeza maandishi mekundu hapa chini. Liverpool vs Everton (LIVE)

Mashabiki wa Napoli wametengeneza toilet paper zenye picha ya Higuan, kisaa …….

Kwa kawaida vilabu vingi vya soka huwa havipendi kuuziana wachezaji mahiri wakiwa wanacheza Ligi moja na mashabiki huwa hawapendi kumuona mchezaji wao anahamia upande wa mpinzani wao katika Ligi, wachezaji wanaofanya hivyo mara nyingi hupoteza heshima yao ndani ya club waliyotoka. Hii ndio imemtokea   Gonzalo Higuan   staa wa zamani wa   Real Madrid   ambaye alihama   Napoli   na kujiunga na   Juventus   timu ambayo ni mshindani wa   Napoli   katika   Serie A , mashabiki wa   Napoli   wanamuona kama msaliti na kesho April 2 2017 anarudi katika uwanja wa   Sao Paulo   wa   Napoli   kwa mara ya kwanza toka ahame timu hiyo. Hapa akiwa Juventus Kama ambavyo mashabiki huwa na heshima kwa wachezaji wao wanaondoka na kujiunga na vilabu vingine, ila kitendo cha kujiunga na   Juventus   Higuan   anahesabika kama msaliti na wameandaa toilet paper zenye picha ya mchezaji...