Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2017

ATCL yakusanya bilioni 9 baada ya kuzinduliwa kwa ndege mbili

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Lasislaus Matindi amesema wamefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 9 kwa miezi minne tu kwa kutumia ndege hmbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Kipindi ndege hizo zinanunuliwa baadhi ya watu walikosoa kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa. Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC). katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena serikalini kwa asilimia 100. SIKILIZA NYIMBO MPYA YA YAMOTO BEND HAPA

SIKILIZA NGOMA MPYA KUTOKA KWA OMG FT BARAKA THE PRINCE UONGO NA UMBEA

OMG wametuletea audio ambaya wamemshilikisha jamaa anayefanya vizuri na nyimbo take achaa aendi Barakah the prince #msanii huyu ambaye yupo chini ya lebo ya rock star 4000  Anfanya vizur sana ndio maana Omg wakaamua kumshirikisha nyimbo inaitwa uongo na umbea  SIKILIZA HAPA

RONALD CRISTIANO AMZIDI KIPATO HASIMU WAKE LIONE MESSI 2016-2017

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameongoza kwa kuwa mwanasoka mwenye kipato zaidi kwa msimu wa 2016-17 hadi sasa. Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12. Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo na Ronaldo anaonekana amepanda haraka baada ya kushinda Ballond’Or. Kiungo mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid. Listi hii hapa MCHEZAJI                        TIMU                              KIPATO Cristiano Ronaldo            Real Madrid                         Pauni 75.62m Lionel Messi     ...

DRAKE BADO ANASHIKILIA USUKANI NA PLAYLIST YA MORE LIFE REKODI

Kweli  More Life  imekuwa tishio kubwa sana na mafanikio makubwa. Baada ya kuachia project yake ya  More Life ,  Drake  amekuwa akiingia kwenye rekodi tofauti tofauti katika ishu ya muziki, ila Good Newz nyingine ni kwamba  Drake  amezizima rekodi mbili za  Billboard  Hot 100  ya kwanza ni  most hits by any solo artist ever (154) na  simultaneous hits on the chart (24). Rekodi zote hizo zimemfanya  Drake kumfunika  Lil wayne  na kumtupa katika nafasi ya pili akiwa na jumla ya entries 135 na 21 debuts, hii inaonyesha jinsi gani kundi la  Young Money  lilivyokuwa tishio kwa sasa,  Nicki Minaj  yeye ndio amekalia kiti na kuvishwa cheo cha mwanamke anayeongoza solo artist. More Life  ndio project ambayo imeshafikisha takribani unit   505,000  za project hiyo na kuifanya kukaa kwenye  Billboard 200  katika wiki yake ya kwanza kushinda ile ya  Views

NEY WA MITEGO AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUTOKA CENTRA JIJI DAR ES SALAAM

Alicho kizungumza nay wa mitego baada ya kuachiwa huru kutokana na Jana kukamatwa aliwa mkoani morogoro na kumpeleka DAR ES SALAAM na Leo kauli ya waziri mwenyezamana kuurusu mwimbo kucheza kwenye vituo vya redio ila ameombwa kuongezea mistari kidogo na kuweka wakepakodi wapo ANGALIA VIDEO HAPO CHINI

Mr T Touch athibitisha kumsaini Young Dee kwenye lebo yake

Mr T Touch amethibitisha kumsajili Young Dee kwenye lebo yake, Touchez Sound Records kwa miaka mitatu. Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV Ijumaa hii kuwa yeye atakuwa anasimamia kutengeneza beat za nyimbo zote za msanii huyo. “Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee. Ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zake zote. Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara,” amesema Touch. Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana naye mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Tumuache Harmorapa afanye yake – Lady Jaydee

Malkia wa Bongo Fleva nchini Lady Jaydee amefunguka kuhusu Harmorapa ambaye amekuwa akiteka vichwa vya habari kutokana na stori zake zikiwemo nyingi za kuvunja mbavu. Jaydee amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa haoni tatizo kwa rapper huyo chipukizi kwa kuwa kila msanii ana njia zake ambazo anatumia za kufikisha sanaa yake inapotakiwa kufika. “Tumuache afanye yake, unajua kila mtu ni ambavyo anaweza kuiwakilisha sanaa yake, kwahiyo mimi naona yuko poa,” amesema muimbaji huyo. Jide ameongeza kuwa alifurahi sana baada ya kuona clip ya video ikimuonyesha Harmo akitoka nduki baada ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuonyeshewa bastola Alhamisi hii SOURCE BONGO5

Huu ni ufafanuzi kutoka Mahakama ya Tanzania kuhusu uteuzi wa Kaimu Jaji Mkuu

Mahakama ya Tanzania imewathibitishia wananchi kuwa itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwa jitihada kubwa bila woga, hofu, huba wala chuki kwa wadau wote kama inavyopaswa. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali ilieza pia kwamba hakuna kosa la kikatiba lililofanywa na Rais John Magufuli kwa kumteua Kaimu Jaji Mkuu kama inavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari. Rais Magufuli Januari 17, mwaka huu alimteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman. Jaji Kiongozi alikuwa anatoa ufafanuzi wa habari iliyochapishwa katika gazeti moja la kila wiki, mwanzoni mwa wiki hii ikiwa na kichwa cha habari ‘Utata Jaji Mkuu.’ Alifafanua katika taarifa yake kwamba kichwa cha habari kilichoelezwa kwenye gazeti hilo kinatoa taswira hasi dhidi ya utendaji wa Mahakama na mchakato wa kupata Jaji Mkuu. Akizungumzia uteuzi wa Kaimu Jaji...

Polisi waanza kumsaka aliyemtolea bastola Mheshimiwa Nape

Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kumsaka mtu aliyemtolea bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Hayo yalisemwa Ijumaa hii na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso. Awali,   Gazeti la Mwananchi   lilimtafuta Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba. Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba. “Sisi tumepokea maelezo ya waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi, hilo ndilo ninaloweza kukwambia,” alisema. Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya polisi aliyevalia kiraia kumtishia bastola, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM). Sambamba na hayo Waziri Nchemba alilaani kitendo hicho na kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Po...

Mr Ttouch aeleza siri ya kutengeza beats za nyimbo nyingi zinazofanya vizuri

Hakuna anayebisha kwamba kwa sasa producer wa ‘Touchez Sound’ Mr Ttouch kuwa ndiye producer anayefanya ngoma nyingi za hivi karibuni ambazo zinafanya vizuri. Mtayarishaji huyo ambaye mpaka sasa ana ngoma kama Komela ya Dayna Nyange, Mazoea ya Billnass, Kibabe ya Professor J, Nisaidie Kushare ya Jay Moe na ngingine nyingi ambazo zinafanya vizuri, ameiambia Bongo5 siri ya kutengeneza beat kali. “Nashukuru Mungu kama mashabiki wameshaanza kusema ninafanya vizuri, hicho ni kitu kizuri sana ambacho kila producer anakitaka,” alisema Mr Ttouch. “Kusema kweli siri ya mafanikio yangu ni kufanya kazi kwa bidii, pia watu wajue mimi siyo msikilizaji wa muziki huu wa kisasa, mimi nyimbo zangu zote nazikiliza nyimbo za zamani, ni nyimbo ambazo zinanipa mambo mengi sana,” Aliongeza,”Mimi nasikiliza ngoma alizo-producer Master J kipindi cha nyuma, P-Funk Majani na maproducer wengine wengi wa zamani. Nikizikiliza kuna vitu fulani ambavyo navipana na vinaweza kunisaidia kuboresha kazi zangu ndi...

Mo Dewji kuificha Simba mikononi mwa Juventus ya Italia

Mohammed Dewji amepanga kuiunganisha Simba kwa Juventus ya Italia. Tajiri huyo namba moja kwa sasa hapa nchini alitua Italia katika klabu hiyo mapema wiki hii na kufanya nao mazungumzo juu ya kuinua soka la Tanzania. Akiongea na mtandao wa Salehjembe, Dewji amesema, “Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo.” Juventus imekuwa ikishirikiana na baadhi ya nchi za Afrika katika kuendeleza mchezo huo ikiwemo Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri. ANGALIA VIDEO YA RAIS WA MISRI YALIYEFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA NA KUACHIWA HURU  

Wanasayansi wagundua kiumbe kingine kinachobadilika rangi kama Kinyonga

Unaweza kutoamini lakini inapofikia wakati ikathibitishwa ni lazima kuamini. Tumekuwa tukiamini kwa kusikia na wakati mwingine kwa kuona kwa macho yetu kuwa   Kinyonga   ndiye kiumbe Pekee anayeweza kubadilisha rangi yake kulingana na mazingira. Leo nimekutana na hii ya Wanasayansi wa   Argentina  ambao wamemgundua   Chura   wa kwanza duniani mwenye uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi yake anapopigwa na mwanga wa jua ambapo wanasayansi hao walisema   Chura   huyo hubadilika kutoka rangi ya   Kahawia   kwenda rangi ya   Kijani   iliyofifia au   Blue   pindi anapokutana na mwanga mkali wa jua. Wanasayansi hao walisema   Chura   huyo hukoza rangi zaidi anapokutana na jua kali zaidi na rangi yake huzidi kupungua akipigwa na mwanga mdogo wa jua wakidai ni jambo ambalo hawakulitegemea ukiwa ni ugunduzi mpya kwao kwa kuwa ni mara chache viumbe wa ardhini kuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi zao. ...

Kidboy: Kumtukana Harmorapa ni sawa na kumpiga chura teke

Pamoja na baadhi ya wadau na mashabiki wa sanaa nchini kuendelea kumtupia maneno machafu msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa, msanii huyo anaonekana kuendelea kung’ara. Producer na mtangazaji mkongwe wa redio na mmiliki wa Tetemesha Production, Sandu Mpaka aka Kidboy, amesema licha ya changamoto ambazo anakutana nazo msanii huyo za kutukanwa na baadhi ya wadau mbalimbali, hali hiyo ndiyo inayosababisha vyanzo tofauti kumzungumzia na watu kumuelewa zaidi. Akizungumza na mtangazaji Manoni MJ wa Pili wa CG FM ya Tabora, Kid amedai kuwa Watanzania wanahitaji burudani za aina tofauti hivyo watu hawatakiwi kuhoji juu ya suala la Harmorapa kupewa airtime kwenye vyanzo vya habari. Msikilize zaidi Kid hapo chini. Audio Player

Bonucci: Napenda tukutane na Barcelona, Bayern ni hatari zaidi

Mchezaji wa klabu ya Juventus Leonardo Bonucci amefunguka kuwa angependa kukutana na Barcelona kwenye mechi za robo fainali ligi ya Mabingwa msimu huu. Juventus wamefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuitoa Porto kwenye michuano hiyo, na Bonucci anatamani droo ya Ijumaa iwakutanishe na Barca ili walipize kisasi cha 2014-15 dhidi ya timu hiyo. “Klabu yetu ni miongoni mwa klabu bora za Ulaya na sasa ni muda wa kwenda mbali iwezekanavyo. Leicester imeshangaza wengi katika michuano lakini mimi binafsi ningependa kukutana ba Barcelona,” Bonucc alisema hayo katika tovuti ya klabu hiyo. “Kukutana na klabu iliyotunyima fursa ya taji miaka miwili iliyopita litakuwa jambo la maana kubwa kwetu. Baada ya kuishangaza PSG, naweza kusema katika timu zilizobaki Barca wapo katika hali nzuri na wanajiamini. “Ambaye hatutaki kukutana naye? Bayern Munich. Kila tunapokwenda [Carlo] Ancelotti anajua namna ya kushinda, kama Guardiola. Ni vema kukutana na Bayern kwenye mechi moja tu ya fainal...

T.I. na Bow Wow wamporomoshea matusi mazito Trump

T.I. na Bow Wow wamemkingia kifua Snoop Dogg kwa kuumporomoshea matusi mazito Rais wa nchi hiyo, Donald Trump. Hatua hiyo ilikuja baada ya Trump kumkosoa Snoop kwa kumkejeli kwenye video ya wimbo wake ambayo inaonesha akimpiga risasi mtu anayefanana na Rais huyo. “Can you imagine what the outcry would be if @SnoopDogg, failing career and all, had aimed and fired the gun at President Obama? Jail time,” aliandika Trump kwenye Twitter. Baada ya kauli hiyo, Bow Wow alimuambia Trump: Ayo @realDonaldTrump shut your punk ass up talking shit about my uncle @SnoopDogg before we pimp your wife and make her work for us.” Naye T.I. ameandika kwenye Instagram:   “@snoopdogg is a Fuckin Legend u Fucking Tangerine Tanned Muskrat scrotum skin, Lacefront Possum fur Wig wearing, Alternative fact, Atomic Dog diarrhea face ass man,” he wrote. “Leave our legends names out ya fuckin old ass puppy piss smelling ass mouth & continue to focus on dividing minorities,building barriers, ali...

MTV base wanapaswa kufanya research zao vizur kabla ya kutaja wasaniiwa kuwaangalia

Miaka 7 iliyopita, Nikikupata ya Ben Pol iliingia kwenye mawimbi ya redio na video yake iliyoongozwa na Adam Juma kubariki macho yetu. Video ya wimbo huo iliwekwa Youtube Oct 7, 2010. Wimbo huo ndio uliomzaa Ben Pol ambaye leo ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania wanaoheshimika. Miaka 7 iliyopita pia, wimbo wa pili (rasmi na wenye mafanikio) wa Diamond, Mbagala, ulitoka. Video yake, iliongozwa pia na Adam Juma na kumpa Diamond nomination ya kwanza kwenye tuzo za MTV MAMA, ya Best New Artist. Kwa Nigeria, miaka 7 iliyopita, alizaliwa pia msanii mwingine ambaye kwa sasa ni maarufu dunia nzima, Wizkid. Akiwa chini ya label ya EME inayomilikiwa na Banky W, aliachia hit single yake Holla at Your Boy (video iliweka Youtube Oct 8,2010, siku moja baada ya Nikukupata ya Ben Pol kuwekwa Youtube). Holla at Your Boy ndio unaofahamika kumtoa na kumtambulisha Wizkid katika jukwaa la muziki Afrika. Mwaka mmoja na nusu baadaye, Afrika ikapata staa mwingine, Davido ambaye wimbo Dami Duro ulio...