Skip to main content

Mr T Touch athibitisha kumsaini Young Dee kwenye lebo yake

Mr T Touch amethibitisha kumsajili Young Dee kwenye lebo yake, Touchez Sound Records kwa miaka mitatu.
Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV Ijumaa hii kuwa yeye atakuwa anasimamia kutengeneza beat za nyimbo zote za msanii huyo.
“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee. Ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zake zote. Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara,” amesema Touch.
Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana naye mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.