Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2017

DIVA AANGUKIA KATIKA PENZI LA MWANAMZIKI WA RNB HERIMZIKI

Diva The Bosslady ametufungulia hadi ndani ya ulimwengu wake mpya wa mapenzi . Amezama, ameoza katika penzi la msanii wa ‘Nakukumbukaga’, Heri Muziki. Jumapili hii ametumia Instagram kuonesha namna alivyokufa na kuzimia kwa muimbaji huyo. Mtangazaji huyo wa Clouds FM amepost video kadhaa akipeana mabusu ya kina Heri. Na hajaaacha kuandika maneno mazito kuonesha anavyompenda muimbaji huyo. “@herimuziki is The Key to My Happiness .. i chose to be Happy   My beib is so damn CUTE Mashaallah   #Lovebirds,” ameandika kwenye video moja. Kwenye nyingine ameandika, “@herimuziki is My Mr. perfect, The Most Handsome, My cute Pie , dope, sexy, Good Kisser , UGH YOUR My Perfect COMBO  YOUR MY WORLD, MY EVERYTHING  you make me so happy,I love you babe so much and I wanna Have your Cute Babies (twins) My Love     #LoveBirds Kwanza @soudybrown keshakupitisha .. hamna namna , shemeji yenu Guys stak maneno zaidi.” Kama kawaida, si wote w...

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.

SUMSUNG YATOA RIPORT YA KUHUSU SABABU ZA KULIPUKA KWA SIMU GALAXY NOTE 7

Kampuni ya Samsung imetoa taarifa yake baada ya kufanya uchunguzi juu ya sababu ya kulipuka kwa simu zake za Galaxy Note 7. Taarifa hiyo imebaini kuwa betri za simu hizo ndio zilizokuwa chanzo cha kulipuka kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye utengenezaji wa betri hizo ambazo zilitengenezwa na mbili ambapo ilitokana mwanzo katika uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa wake. Ripoti hiyo imeongeza kuwa matatizo mengine yalitokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutokaa vizuri katika sehemu yake ya ndani ya simu. Simu hizo zilisitishwa kuuzwa mwezi Oktoba mwaka jana huku ikikadiriwa kuwa simu hizo tayari zilikuwa zimeuza kiasi cha dola bilioni 5.3 duniani kote.

MCHEZAJI WA NICE YA UFARANSA AMESEMA ALIKUA MWATHIRIKA WA UBAGUZI WA RANGI

Mchezajiwa wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia. Balotelli ambaye mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 aliandika katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua? ”Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa”. Balotelli ambaye alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi waliyo toka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo. Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote. Balotelli amesha funga mabao 10 katika mechi 15 tangu alivyo jiunga na ...

BAADA YA MAFUA YA NDEGE KUGUNDULIKA NCHI YA UGANDA HAYA NI MAMBO SABA YA KUFUATILIA ILI KUEPUKA

Baada ya ugonjwa wa mafua ya ndege kugundulika nchi jirani ya Uganda baada ya kuwepo kwa vifo vingi vya ndege pori katika maeneo  ya Lutembe beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga na Bukakata na vifo hivyo kutokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata) na inahisiwa kuwa ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege pori wanaohama kutoka nchi za Ulaya. Baada ya taarifa hizo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo January 18 2017 imetoa taarifa kuhusu kuwepo kwa virusi vya mafua makali ya ndege katika nchi jirani ya Uganda.  Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo yalioathirika ni maeneo yanayozunguka ziwa Victoria pamoja na ziwa lenyewe. Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya imesema kuwa hadi sasa hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo huko nchini Uganda hivyo wametoa tahadhari  kuwa  kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa kusambaa kwa binadamu ikiwa hatua madhubuti  za kujikinga hazitazi...

NAY WA MITEGO AANDIKA KUA HAJA WAI KUONA NYIMBO MBAYA KAMA ZILIZO TOKA JANA HARAFU AKASEMA MTAG KAMA UNA MJUA MASHABIKI WENGI WALI MTAG MADEE

Wafalme wa Manzese, Madee na Nay wa Mitego, wameirejesha tena bifu yao. Imerudi upya baada ya Madee kuandika mstari kwenye wimbo wake mpya, Hela ambao umetafsiriwa kumwendea hasimu wake, Nay. “Yule kijana wa home sio staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa,” Madee amerap kwenye wimbo huo. Baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, Nay aliandika kwenye Instagram, “Leo nimesikia Wimbo Mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia Mwaka huu.” “Mtag uyo Msanii mwenye huo wimbo Kama ushausikia..?!”

KABLA SIJAANDI WIMBO WA MOYO SUKUMA DAMA NILIFANYA UTAFITI KUJUA KAZI YA MOYO.....DITTO

Hit maker wa wimbo ‘Moyo Sukuma Damu’ Lameck Ditto amedai kabla hajaandika wimbo huo alianza kufanya utafiti ili kujua kazi ya moyo. Muimbaji huyo ambaye pia ni muandishi mzuri wa nyimbo, alikiambia kipindi cha Yaliyomo Yamo Cha Radio One Stereo kuwa asingeweza kuandaa wimbo huo vizuri bila kufanya utafiti wa kile alichokizungumza. “Kabla sijaimba Moyo Sukuma Damu, nilifanya research kujua kazi ya moyo,” alisema Ditto. Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi umekuwa sana, mashabiki wanasikiliza neno hadi neno, kwahiyo suala la utafiti kama unaweza kufanya ni bora ufanye ili kuboresha zaidi muziki wako,” Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wachache waliorudi kwa kishindo kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

RAIS WA ZAMANI WA MAREKAN GEORGE H.W BUSH ALAZWA HOSPITALIN

Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush amekimbizwa katika hospitali ya Houston Methodist ya mjini Texas baada ya kuzidiwa ghafla. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mkuu wa wafanyikazi wa rais huyo wa 41 wa nchi hiyo, Jean Becker kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na kuna uwezekano mkubwa akaruhusiwa kutoka hospitalini siku chache zijazo. Siku chache zilizopita mtoto wake George W. Bush ambaye na yeye aliwahi kuwa Rais Marekani alitoa ripoti kuwa atahudhuria sherehe za kuapishwa Donald Trump huku akiongeza kuwa baba yake, George H.W., hatohudhuria kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.

YAHAYA TOURE AMEKATEA KWENDA CHINA

Mchezaji wa klabu ya Manchester City Yaya Toure inasemakana kuwa amekataa ombi la mshahara wa paundi 430,000 kwa wiki kutoka China. Toure ambaye ana umri wa miaka 33 amevutia timu nyingi katika ligi ya China ,wakati ilipoonekana kwamba huenda asishirikishwe katika mechi zozote na kocha Pep Guardiola. Aliamua kutoondoka wakati huo na akakataa tena alipopewa kitita hicho wakati wa dirisha hili la uhamisho. Mkataba wa raia huyo wa Ivory Coast unakamilika msimu huu. Amekuwa mchezaji muhimu wa City tangu aliporudishwa katika kikosi cha kwanza na alianza mechi yake ya saba mfululizo wakati wa kushindwa kwa 0-4 dhidi ya Everton katika mechi ya ligi ya Uingereza hapo Januari 15. Toure amekuwa huru kuingia katika mkataba na vilabu vingi ughaibuni tangu mwezi Januari lakini imedaiwa kwamba bado anapenda ligi ya Uingereza. Toure bado hajapata hakikisho lolote kuhusu mkataba wake kutoka kwa kocha wake Guardiola.

PICHA ZILIVYO MFANYA STAA KCEE WA NIGERIAAWE GUMZO MTANDAONI

Ikiwa weekend ndio inaraibia kuisha na kama kawaida huwa sipendi upitwe na chochote kinacho trend kwenye mitandao ya kijamii. Leo January 15 2017 nimekutana na stori ya staa muimbaji  KCEE  wa  Nigeria  ambaye amedaiwa kuwa na amekuwa akizifanyia photoshop (kuedit picha kwa utaalamu ili kuonyesha uhalisia tofauti) baadhi ya picha zake. Ni kawaida kuedit picha lakini pale ambapo inaonekana kupoteza uhalisia kabisa inakuwa ishu nyingine. Mtandao wa habari za burudani wa Marekani wa  Theshaderoom.com  umeandika kuwa baadhi ya picha ambazo msanii huyo amekuwa akipost sio za kweli haswa ile ambayo ameonekana yuko na  Christiano Ronaldo . TSR STAFF: Talia O. @theclosetratchet on Instagram & @tallyohhh on Twitter! Roommates, have any of you ever used photoshop to touch up a blemish on your face or to make the background of your image more lively? Well, TheNet.Ng is questioning #Naija singer #Kcee’s Instagram photos, because it looks like...
Mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya ambaye amekuwa na uthubutu wa kuzirudia na kuziigiza movie na nyimbo za mastaa mbalimbali. Safari hii ameirudia movie ya ‘The gods must be crazy’ na ameeiita ‘The Gods are not crazy we are’, tazama hapa chini alafu toa komenti yako.

MASHABIKI WA MUZIKI KENYA WAMLILIA DARASSA

Mashabiki wa muziki wa nchini Kenya wamemlilia Darassa. Hilo limedhihirika katika ujumbe aliouandika muimbaji wa nchi hiyo, Nyota Ndogo kwenye mtandao wa Instagram. Kupitia mtandao huo, Nyota Ndogo aliweka picha ya mashabiki na kuandika, “@darassacmg plz kuna pesa zako kenya zinakungoja.this was my show in malindi.nimemaliza kupiga show mashabiki wanamuomba dj acheze nyimbo yako na mimi ni dance.nipo na video yani mimi ni dance.kimbia huku mara moja kabla nyimbo haijaisha ufanye tour ongea na @gatesmgenge nimzuri wakupiga debe.unamashabiki sio tz pekeake.do it now.” Hizi ni comment za mashabiki katika mtandao huo: gatesmgenge:  @nyota_ndogo tayari mpangilio wafanywa tayari tushazungumza na @hanscana_ karibuni watu wangu wa #Malindi. ulomchokoza: _kaja@darassacmg@darassacmg @darassacmg plzzzzzzz bro pitia hapa cntermourice:  Wimbo wa taifa unaliliwa kenya @blaze_tz omoyut:  @darassacmg ukuje huku SIKILIZA SONG JIPYA KUTOKA KWA AUSTIN

MUSIC;AUGUST ALSINA-DRUGS

Outside of his appearance on DJ Khaled’s gold-certified single “Do You Mind,” August Alsina remained relatively quiet in 2016. But the New Orleans crooner is back with new music for the new year. On the mellow “Drugs,” Alsina sings about a girl who he just can’t shake. “I can’t get enough of your drugs,” he croons. “So baby, just tell me when you’re ready.” Expect more music from Alsina in the coming months. He is working on his third album, the follow-up to 2015’s This Thing Called Life. ANGALIA HAPA CHINI  HII VIDEO

WAJERUMANI WASHAURIWA KUTEMBEA KAMA NDEGE PENGUINI ILI KIJIKINGA NA AJALI

Madaktari nchini Ujerumani wamewashauri raia kutembea kama ndege aina ya Penguin kwa lengo la kuepuka kuteleza na kuanguka katika kipindi hiki cha baridi jambo linalotokana na kuganda kwa barafu baraabarani. Madaktari nchini Ujerumani wamewashauri raia watembee kama ndege aina ya penguin katika kipindi hiki cha baridi kali lenye kuandamana na kuanguka kwa theluji ambazo baadae zinaganda na kuwa barafu katika maeneo mengi ya barabara. Kitengo cha utabiri wa hali ya hewa kimesema hali hiyo itaendelea kwa siku kadhaa na kwamba aina hiyo ya kutembea inayomsadia kiumbe huyo anaeishi katika maeneo ya baridi kali, inaweza kuwanusuru watu na hatari ya kuvunja viungo vyao. Ushauri huo uliosambazwa kupitia tovuti ya chama cha watoa tiba ya mifupa nchini Ujerumani na ushauri na nasaha unasema kutembea kwa kunyata kunakufanywa na aina ndege huyo, kunaweza kusaidia kukabiliana na kuteleza katika barabara zenye barafu. Lakini kama binadamu atatembea kwa namna yake ya kawaida ni rahi...