Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2017

NIKKI WA PILI AMESEMA MZIKI WA ZAMANI ULIKUA UNA PIMWA NA VITU VINGI TOFAUTI NA WA SASA

Nick wa Pili ametaja vitu ambavyo kwa sasa vinafanya muziki uonekane mzuri tofauti na ilivyokuwa zamani. Rapper huyo kupitia mtandao wa Twitter ameandika ujumbe unaoonyesha vitu hivyo ambapo moja wapo ni views za video, followers na vingine. Kupitia mtandao huo, Nick ameandika, “Miaka ya 90’s ubora wa muziki ulikuwa unapimwa na vitu vingi, sasa kipimo ni kimoja, number views,money,rotation,downloads,chati,followers..” Kwa mujibu wa ujumbe huo wa Nick unaweza ukaona kuwa muziki wa zamani ndio ulikuwa bora zaidi kwakuwa vitu hivyo havikuwepo lakini mpaka leo hii bado zinaendelea kufanya vizuri.

JOKATE AKUTANA NA JAY Z BEYONCE NA MTOTO WA JAYZ BLUE IVY KWENYE MCHEZO WA NBA ALLSTARS GAME

Kukutana na Jay Z na Beyonce ni suala gumu, kukutana nao na ukashikana nao mikono na kuzungumza mawili matatu nao ni suala gumu zaidi. Lakini bahati hiyo ya mtende imeamuangukia mrembo wa Tanzania, Jokate Mwegelo Jumapili hii . Siamini: Jokate Mwegelo akisalimia na Jay Z huku mtoto wake, Blue Ivy akiamtazama kwa makini. Pembeni yao ni Queen Bey Jojo amefanikiwa kukutana na The Carters wakiwa na mtoto wao, Blue Ivy kwenye mchezo wa NBA All-Star Game uliofanyika Jumapili mjini New Orleans, Louisiana kwenye uwanja wa Smoothie King Center. “So NBA Africa took me courtside and I haaaaaaad to say hello to the Carters,” ameandika Jokate. “OMG  . @beyonce is super cute and I can’t believe she shook my hand and was like nice to meet you.  . I was like wait I need a picture, I came all the way from Tanzania for this B  . She’s so sweeeeeet and I’m so lucky lmao,” ameongeza. “Thank you @beylite @balleralert for this pic I couldn’t snap one as I was shocked and s...

VANESSA MDEE NA ICE PRINCE WATUMBUIZA KWENYE BBA NAIJA

Vanessa Mdee na rapper wa Nigeria, Ice Prince Zamani jana wametumbuiza kwenye show ya Big Brother Naija 2017. Wawili hao wanafanya vizuri na wimbo wao No Mind Em. Baada ya show hiyo Ice aliweka picha hiyo juu na kuandika: 1 for TV !!! @vanessamdee Thank You sister #NoMindDem  .” ANGALIA VIDEO YA MANJI AKIWA ANAENDA CENTRAL

mewaambia Sony Music mashabiki wangu wako active sana, tusiwaangushe tena

EET 1   SHARE TW COMMENTS Alikiba ameyasikia malalamiko ya mashabiki wake kuhusu ukimya wake wa hapa na pale na amekiri huumia sana kuona wakimrushia lawama. Kutokana na ukweli huo, hitmaker huyo wa Aje amedai kuwa amelazimika kuwaambia mabosi wa Sony kuwa wajipange vyema ili kuhakikisha kuwa mashabiki wake wanaridhika. Kwenye interview na millardayo.com, Alikiba amedai kuwa CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson, ameiambia bodi ya label hiyo jinsi Alikiba alivyo na mashabiki wengi nyuma ambao panapotokea kuchelewa kwa lolote, ‘hung’ata kama nyuki.’ “Kwahivyo they have to make sure kila kitu kinaenda on point, kila kitu hakitakiwi kudelay, kila kitu kinakwenda sawa,” amesema Kiba. Alikiba akiteta jambo na CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson “Yaani they have to make sure kwamba hawadisappoint fans wangu, kwasababu pressure ambayo wanapata yaani tayari Sean ameelewa kwahiyo wamekubali wamesema sawa, nadhani fans kitu hicho sasa ni...

Alikiba - AJE Remix (Official Video)

video ya  king wa bongo flave Alikiba ametusogezea hii remix akimshilikisha msanii kutoka Nigeria M.I

VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA WATOTO HAWA WASIKITISHA WENGI VIDEO

Moja kati ya jambo lililowasikitisha wengi Jumatatu hii katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni pale walipotajwa watoto wawili wa kike ambapo mmoja ana umri wa miaka 14 na mwingine 16 kuwa walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka mitano. Wakati huo huo mtoto mmoja mwenye miaka 16 aliongeza kuwa mbali na kutumia madawa hayo lakini pia yamempelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kuwa wakati mwingine ilimlazimu kujiuza ili apate fedha za kununulia dawa hizo. Wakati huo huo Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya, Rogers Sianga ameahidi kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia huduma bora za afya ambazo zitawasaidia wasirudi tena kwenye janga hilo. Orodha hiyo ya tatu iliyotolewa leo na Mh. Makonda ina idadi ya majina 97 ambapo kati yao amedai kuna majina ambayo yatawasha moto zaidi huku akiahidi kuwa kuna awamu nyingine nne zimebakia za kutoa majina hayo.

WAZIRI MKUU AAGIZA MAENEO YA MAGEREZA YAPIMWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka. Ametoa agizo hilo leo mchana katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma. “Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza. Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo. “Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapi...

Baada ya wema sepetu kutoka kwa mdhamana hi I leo

Mamnia ya watu walikuepo mahakama ya kisutu kusubilia hukumu ya wema sepetu ambayo ilikua imebamba kila kona watu wakimuombea awezekutoka salama na maombi yao yamefanikiwa nakuweza kutimia ANGALIA VIDEO HAPA YA WEMA AKIWA AMETOKA MAHAKAMANI

MANJI AMWAGA MAMILION KWENYE GOOGLE ADS KUJISAFISHA SIKU MOJABAADA YA KUTAJWA KWENYE ORODHA MPYA YA MAKONDA

Siku moja baada ya mfanyabiashara maarufu na mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye orodha ya pili ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, amemwaga mamilioni ya fedha kulipia matangazo ya mtandaoni, google ads kujisafisha. Matangazo hayo yanaonekana kwenye tovuti nyingi, hata za nje unazozifungua kuanzia Alhamis hii. Hatua hiyo pia imekuja saa chache baada ya Manji kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia kutajwa kwake ambako alisema amedhalilishwa na kwamba ataenda polisi Alhamis hii badala ya Ijumaa kama ambavyo Makonda aliwataka. Matangazo hayo yanaonesha bango lenye picha yake na maelezo yasemayo  ‘Yes I ‘am addicted to Yanga.’ Ukiclick, inakupeleka kwenye maelezo marefu yanayomwelezea mfanyabiashara huyo pamoja na mambo aliyoyafanya. Maelezo hayo ni kama yafuatayo: Manji Mwenyekiti wa kihistoria Yanga MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, Yus...

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA

Today January 31 2017 the Council of Tanzania exams’ NECTA has declared the results of Form IV ‘CSEE 2016’ and the result of the test of knowledge (QT) 2016. CLICK HERE  For Results Of Form IV   CSEE 2016  ( FORM IV   CSEE 2016 ) You can also see the results of the test results of knowledge (QT) 2016. CLICK HERE  For Results Of  (QT) 2016

DAVIDO AMLUDISHA MENEJA WAKE WA ZAMANI

Davido amemrejesha kazini meneja wake wa zamani kabla ya Kamal Ajiboye aliyemfuta kazi mwezi uliopita kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuyumba kwa biashara na matumizi mabaya ya pesa. Kupitia Twitter, Davido amemtangaza Asa Asika kuwa meneja wake mpya kwa sasa, “Welcome back yellow MAN @AsaAsika ! BACK TO BASICS!” Asa Asika aliwahi kuwa meneja wa msanii huyo mwaka 2012 lakini baadaye walitibuana kwa sababu hizo hizo za masuala ya kibiashara.

SADIO MANE ASAFIRISHWA KWA NDEGE BINAFSI

Klabu ya Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya binafsi mshambuliaji wao Sadio Mane, baada ya  timu yake kutolewa katika michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kuwahi kucheza mechi ya ligi na Chelsea. Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakati wa mechi ya robo fainali siku ya Jumamosi. Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo. Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu Mane alivyo enda kushiriki mechi za kimataifa. Walipoteza na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves. SIKILIZA NYIMBO MPYA YA COUNTRY WIZZY FT GODZILLAH