Klabu ya Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya binafsi mshambuliaji wao Sadio Mane, baada ya timu yake kutolewa katika michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kuwahi kucheza mechi ya ligi na Chelsea.
Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakati wa mechi ya robo fainali siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.
Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu Mane alivyo enda kushiriki mechi za kimataifa.
Walipoteza na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.
SIKILIZA NYIMBO MPYA YA COUNTRY WIZZY FT GODZILLAH
Comments
Post a Comment