Skip to main content

KOCHA WA ARGENTINA ALICHOKISE KUHUSIANA NA LIONEL MESSI

Moja kati ya vipindi vigumu kwa staa wa soka wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona Lionel Messi ni kipindi hiki ambacho Argentina haifanyi vizuri sana, Lionel Messi ambaye ni nahodha wa Argentina aliwahi kulaumiwa na kuandikwa kuwa hajitumi timu ya taifa.
Lionel Messi pia amewahi kutuhumiwa kuwa amekuwa na sauti katika uchaguzi wa wachezaji wa timu ya taifa mbele ya kocha wao Edgardo Bauza madai ambayo kocha Bauza amekuwa akiyapuuzia na kukaa kimya.
lavanguardia_g_874703504-k7ub-u301455491366e5b-992x558lavanguardia-web
Maxi Lopez kushoto akiwa na Lionel Messi wakati wakiwa FC Barcelona
Kocha Bauza ameamua kuzungumzia kuhusiana na maneno hayo “Kwa wale wanaofikiria kuwa Lionel Messi anachagua wachezaji wa kuunda kikosi cha timu ya taifa, sidhani kama kuna haja ya kuwajibu, kama Messi akichagua wachezaji basi nitakuwa nje ya timu”
Kama utakuwa unakumbuka October 14 Lionel Messi alidaiwa kuhusika na kuzuia mchezaji Mauro Icardi asiitwe timu ya taifa, kwa sababu alimchukua mke wa mchezaji mwenzake wa Argentina na rafiki yake ambaye amewahi kucheza nae FC BarcelonaMaxi Lopez.
0012709961

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.